1. Tumsifu Mungu wetu
Aliye mbinguni,
Atawala kwa dhamira,
Mbingu nazo nchi.
Jina lake liinue;
Sifu utawala!
Msujudu Bwana Mungu,
Mfalme daima.
2. Chini yake, kwa amriye,
Sayari na mbingu
Huonyesha kila saa
Hekima ya Mungu.
Jina lake liinue;
Sifu utawala!
Msujudu Bwana Mungu,
Mfalme daima.
3. Ua dogo liishilo,
Ndege wa msimu,
Nao pia wanatunzwa;
Kawaumba Mungu.
Jina lake liinue;
Sifu utawala!
Msujudu Bwana Mungu,
Mfalme daima.
4. Sauti za kuvutia
Nyimbo zimwimbie;
Tumsifu, sala zetu
Azijibu zote.
Jina lake liinue;
Sifu utawala!
Msujudu Bwana Mungu,
Mfalme daima.
Maandishi: Ada Blenkhorn, 1858–1927
Muziki: Alfred Beirly, 1848–1929