Book cover

Tumsifu Mungu Wetu

Nyimbo za Dini, 34

0:00 0:00
Introduction
All Verses

1. Tumsifu Mungu wetu Aliye mbinguni, Atawala kwa dhamira, Mbingu nazo nchi.

Jina lake liinue; Sifu utawala! Msujudu Bwana Mungu, Mfalme daima.

2. Chini yake, kwa amriye, Sayari na mbingu Huonyesha kila saa Hekima ya Mungu.

Jina lake liinue; Sifu utawala! Msujudu Bwana Mungu, Mfalme daima.

3. Ua dogo liishilo, Ndege wa msimu, Nao pia wanatunzwa; Kawaumba Mungu.

Jina lake liinue; Sifu utawala! Msujudu Bwana Mungu, Mfalme daima.

4. Sauti za kuvutia Nyimbo zimwimbie; Tumsifu, sala zetu Azijibu zote.

Jina lake liinue; Sifu utawala! Msujudu Bwana Mungu, Mfalme daima.