Number 40
Mungu Yu Nanyi Wapendwa
Mungu Yu Nanyi Wapendwa
1. Mungu yu nanyi wapendwa,
Kutwa akiwalinda.
Apenda kuwabariki,
Mtapotenda mema.
Abariki, abariki,
Kama mtaamini.
2. Nao malaika juu
Waona kazi zenu,
Na wanaandika yote
Mema, hata maovu.
Penda wema! Penda wema!
Mungu akubariki.
3. Mungu anatufundisha
Kwa sauti ya Roho.
Sikiliza ushawishi,
Uwe furaha yako.
Aminika, aminika
Kwa Mungu na Sayuni.
Maandishi: Charles L. Walker, 1832–1904
Muziki: John Menzies Macfarlane, 1833–1892