1. Bwana ni nuru; ya nini hofu? Wakati wote yupo karibu. Ni wokovu wangu toka dhambini; Na Roho hunipa ahadi hii.
Bwana ni nuru; Ni wimbo na furaha. Siku, usiku, Naongozwa daima.
2. Bwana ni nuru; hushinda giza. Imani kuu, mbingu hupenya Ambapo daima ni Mwenye enzi. Hivyo kwa nini nibaki gizani?
Bwana ni nuru; Ni wimbo na furaha. Siku, usiku, Naongozwa daima.
3. Bwana ni nuru; ni nguvu yangu. Kwa nguvu yake nitayamudu. Mapungufu yangu huimarisha, Kwa uaminifu nabarikiwa.
Bwana ni nuru; Ni wimbo na furaha. Siku, usiku, Naongozwa daima.
4. Bwana ni nuru, yote hakika. Kwake hakuna giza kabisa. Mkombozi wangu, Mfalme wangu. Nitamsifu na watakatifu.
Bwana ni nuru; Ni wimbo na furaha. Siku, usiku, Naongozwa daima.