1. Karibu na Ewe, Mungu wangu! Ingawa mateso Ni machungu, Bado wimbo wangu: Karibu na Mungu Karibu na Ewe, Mungu wangu!
2. Ningali njiani Kumekuchwa, Jiwe ndilo mto, Nasinzia. Naota usiku: Karibu na Mungu Karibu na Ewe, Mungu wangu!
3. Ngazi za mbinguni Wazishusha; Unanipa yote Kwa neema; Waniita juu Karibu na Mungu Karibu na Ewe, Mungu wangu!
4. Kukicha nasifu, Wastahili; Nayosimamisha Ni Betheli, Kama kumbukumbu; Karibu na Mungu Karibu na Ewe, Mungu wangu!
5. Kisha kwa furaha Nikipaa, Nifike mbinguni Kwako tena. Bado wimbo wangu: Karibu na Mungu Karibu na Ewe, Mungu wangu!