1. Karibu na Ewe,
Mungu wangu!
Ingawa mateso
Ni machungu,
Bado wimbo wangu:
Karibu na Mungu
Karibu na Ewe,
Mungu wangu!
2. Ningali njiani
Kumekuchwa,
Jiwe ndilo mto,
Nasinzia.
Naota usiku:
Karibu na Mungu
Karibu na Ewe,
Mungu wangu!
3. Ngazi za mbinguni
Wazishusha;
Unanipa yote
Kwa neema;
Waniita juu
Karibu na Mungu
Karibu na Ewe,
Mungu wangu!
4. Kukicha nasifu,
Wastahili;
Nayosimamisha
Ni Betheli,
Kama kumbukumbu;
Karibu na Mungu
Karibu na Ewe,
Mungu wangu!
5. Kisha kwa furaha
Nikipaa,
Nifike mbinguni
Kwako tena.
Bado wimbo wangu:
Karibu na Mungu
Karibu na Ewe,
Mungu wangu!
Maandishi: Sarah F. Adams, 1805–1848
Muziki: Lowell Mason, 1792–1872