Number 49
Niongoze
Niongoze
1. Yesu, Mkombozi,Niongoze.Nakata shauri,Niongoze.Hata kwenye giza,Na kunapokucha.Uwe wangu mwanga.Niongoze.
2. Hata kwenye shida,Niongoze.Nifundishe wema.Niongoze.Nguvu ya wokovuIwe kila siku,Bwana, kinga yangu.Niongoze.
3. Niwapo na dhambi,Niongoze.Nikiwa na jonzi,Niongoze.InapotowekaAmani na raha,Nijaze neema,Niongoze.
4. Kikifika kifo,Niongoze.Nitulize moyo.Niongoze.UnihurumieIli upendoweKwako unilete.Niongoze.
Maandishi na muziki: Orson Pratt Huish, 1851–1932