Book cover

Nifuate

Nyimbo za Dini, 57


0:00 0:00
Introduction
All Verses

1. “Nifuate,” alisema. Nyayo zake kufuata, Tuwe pamoja naye tu Mwana Mpendwa wa Mungu.

2. “Nifuate,” semi fupi, Bali mwanga wa ukweli Upo kwenye hili neno Ili kuwatia moyo.

3. Je, yatosha tu kujua Twapaswa kumfuata, Kwenye bonde la machozi? La hasha, hata mbinguni.

4. Siyo tu kumfuata Tukiwa kwenye dunia, Hata tukiwekwa huru Na Bwana turithi mbingu.

5. Ni lazima kuisaka Njia ya kuendelea Kumtafuta Mwokozi Katika yoyote hali.

6. Enzi, himaya na nguvu, Na utukufu ni vyetu, Tukilitii milele, Neno lake, “Nifuate.”