Number 57
Nifuate
Nifuate
1. “Nifuate,” alisema.Nyayo zake kufuata,Tuwe pamoja naye tuMwana Mpendwa wa Mungu.
2. “Nifuate,” semi fupi,Bali mwanga wa ukweliUpo kwenye hili nenoIli kuwatia moyo.
3. Je, yatosha tu kujuaTwapaswa kumfuata,Kwenye bonde la machozi?La hasha, hata mbinguni.
4. Siyo tu kumfuataTukiwa kwenye dunia,Hata tukiwekwa huruNa Bwana turithi mbingu.
5. Ni lazima kuisakaNjia ya kuendeleaKumtafuta MwokoziKatika yoyote hali.
6. Enzi, himaya na nguvu,Na utukufu ni vyetu,Tukilitii milele,Neno lake, “Nifuate.”
Maandishi: John Nicholson, 1839–1909
Muziki: Samuel McBurney, 1847–1909