1. Japo kuna matatizo,Jikazeni kwa bidii!Na siku ya ufufuoItaeneza ukweli,Itaeneza ukweli.
2. Japo shida zatuzonga,Punde muda si mrefu,Kristo atakuja tena,Na wingi wa utukufu,Na wingi wa utukufu.
3. Msifuni Mungu kwa nyemi;Furaha yenu idumu.Japo bado kuna dhiki,Amani ipo kwa Yesu,Amani ipo kwa Yesu.
4. Japo tumedhulumiwa,Na kuporwa na adui,Ipo ahadi ya Bwana;Azma yake haikomi,Azma yake haikomi.
5. Kazi yasonga kwa kasiKwa matukio makuu,Ufalme wa zama hiziUtajaza ulimwengu,Utajaza ulimwengu.
6. Japo mwovu atanuna,Maneno ya manabiiYatasimama imara;Hakuna wa kubatili,Hakuna wa kubatili.
7. Litukuzwe lake jina,Atumaye watumishiKuambia mataifaHabari ya ukombozi,Habari ya ukombozi.