Auto-scroll is most reliable with MIDI (computer-generated) audio.
Practice
Loading…
Kristo Mwokozi
1. Kristo Mwokozi ni Mfalme!Naimba kwa moyo wote;Kwa furaha nitasifu,Niseme amina kuu.Kristo Mwokozi; ndiye Neno.Aliishi kati yao,Alifanya miujizaTulisifu lake jina.
2. Kristo Mwokozi; ndiye Bwana!Alikuja kutawalaKati yao, wanadamu,Na dhambi awanusuru.Kristo Mwokozi; ndiye nija.Karithi yote ya Baba,Asema: “Njooni kwangu,Na ninyi muwe na Mungu.”
3. Kristo Mwokozi — Bwana, Mungu!Neno lake lina nguvu.Nitamwabudu kwa dhati;Ndiye chanzo cha ukweli.Kristo Mwokozi ni dhamana.Kwa Shetani hunitoa.Nitaishi kwa upendoKule mbinguni alipo.
4. Kristo Mwokozi ni Muumba!Kwake ndoto natimiza;Nipitapo kwenye dhiki,Ye husema: “Utastawi.”Kristo Mwokozi niwe nayeSiku hiyo, kwa vyovyote,Akija kwa walimwenguKutawala kati yetu.