Book cover

Hamu ya Nafsi ni Sala

Nyimbo za Dini, 77


0:00 0:00
Introduction
All Verses

1. Hamu ya nafsi ni sala, Usemi halisi, Kama moto, ni hisia, Yawaka moyoni.

2. Pumzi hushushwa na sala, Hufuta machozi. Macho juu hutazama Kwa Mungu Mwenyezi.

3. Lugha nyepesi ni sala, Hata kwa mtoto. Wimbo unaovutia Mfalme alipo.

4. Sala kweli ni uhai; Kwa mkristo, hewa. Mlangoni mwa mauti Huenda kwa sala.

5. Sauti ya mwenye dhambi, Akianza toba, Malaika wafurahi Kila akiomba.

6. Watakatifu makini Kupitia sala, Waupata ushiriki Wa Baba na Mwana.

7. Tuombapo, si sisi tu; Na Roho aomba, Na Yesu kitini juu Anatuombea.

8. Ewe uliye Ukweli, Njia na Uzima. Uyajuaye maombi Tufunze kuomba.