1. Hamu ya nafsi ni sala,
Usemi halisi,
Kama moto, ni hisia,
Yawaka moyoni.
2. Pumzi hushushwa na sala,
Hufuta machozi.
Macho juu hutazama
Kwa Mungu Mwenyezi.
3. Lugha nyepesi ni sala,
Hata kwa mtoto.
Wimbo unaovutia
Mfalme alipo.
4. Sala kweli ni uhai;
Kwa mkristo, hewa.
Mlangoni mwa mauti
Huenda kwa sala.
5. Sauti ya mwenye dhambi,
Akianza toba,
Malaika wafurahi
Kila akiomba.
6. Watakatifu makini
Kupitia sala,
Waupata ushiriki
Wa Baba na Mwana.
7. Tuombapo, si sisi tu;
Na Roho aomba,
Na Yesu kitini juu
Anatuombea.
8. Ewe uliye Ukweli,
Njia na Uzima.
Uyajuaye maombi
Tufunze kuomba.
Maandishi: James Montgomery, 1771–1854
Muziki: George Careless, 1839–1932