1. Baki nami; kumekuchwa. Muda ni jioni; Giza sasa laingia; Haliepukiki. Moyoni mwangu, mwalikwa, Kaa nami kwangu.
Mwokozi baki na mimi; Ona, kumekuchwa. Mwokozi baki na mimi; Ona, kumekuchwa.
2. Baki nami; kumekuchwa. Kuwapo pamoja Kumegusa moyo wangu, Tulipoongea. Umejaza nafsi yangu Kwa kuwa karibu.
Mwokozi baki na mimi; Ona, kumekuchwa. Mwokozi baki na mimi; Ona, kumekuchwa.
3. Baki nami; kumekuchwa. Usiku mpweke Kama hutanena nami, Uniangazie. Giza, linanitishia, Kuingia kwangu.
Mwokozi baki na mimi; Ona, kumekuchwa. Mwokozi baki na mimi; Ona, kumekuchwa.