1. Baki nami; kumekuchwa.
Muda ni jioni;
Giza sasa laingia;
Haliepukiki.
Moyoni mwangu, mwalikwa,
Kaa nami kwangu.
Mwokozi baki na mimi;
Ona, kumekuchwa.
Mwokozi baki na mimi;
Ona, kumekuchwa.
2. Baki nami; kumekuchwa.
Kuwapo pamoja
Kumegusa moyo wangu,
Tulipoongea.
Umejaza nafsi yangu
Kwa kuwa karibu.
Mwokozi baki na mimi;
Ona, kumekuchwa.
Mwokozi baki na mimi;
Ona, kumekuchwa.
3. Baki nami; kumekuchwa.
Usiku mpweke
Kama hutanena nami,
Uniangazie.
Giza, linanitishia,
Kuingia kwangu.
Mwokozi baki na mimi;
Ona, kumekuchwa.
Mwokozi baki na mimi;
Ona, kumekuchwa.
Maandishi: M. Lowrie Hofford, 1823–1888
Muziki: Harrison Millard, 1830–1895