1. Yavutia kuuimba Upendo wake Muumba, Alikuja—ni ajabu— Kuokoa wanadamu.
Kwani, Yesu alikufa, Kuwakomboa wafungwa. Hivyo hosana ziimbwe; Nyote kiri upendowe.
2. Ni vyema kila Sabato, Kama lilivyo agano, Kuzikumbuka alama, Imani kufanya upya.
Kwani, Yesu alikufa, Kuwakomboa wafungwa. Hivyo hosana ziimbwe; Nyote kiri upendowe.
3. O! Wasaa mtukufu! Wote kuwa na walimu, Kuadhimisha upendo Na kuuenzi kwa nyimbo.