Number 96
Yavutia Kuuimba
Yavutia Kuuimba
1. Yavutia kuuimbaUpendo wake Muumba,Alikuja—ni ajabu—Kuokoa wanadamu.
Kwani, Yesu alikufa,Kuwakomboa wafungwa.Hivyo hosana ziimbwe;Nyote kiri upendowe.
2. Ni vyema kila Sabato,Kama lilivyo agano,Kuzikumbuka alama,Imani kufanya upya.
Kwani, Yesu alikufa,Kuwakomboa wafungwa.Hivyo hosana ziimbwe;Nyote kiri upendowe.
3. O! Wasaa mtukufu!Wote kuwa na walimu,Kuadhimisha upendoNa kuuenzi kwa nyimbo.
Kwani, Yesu alikufa,Kuwakomboa wafungwa.Hivyo hosana ziimbwe;Nyote kiri upendowe.
Maandishi: George Manwaring, 1854–1889
Muziki: Ebenezer Beesley, 1840–1906
Jina la tuni: HANCOCK