Book cover

Yesu, Mkombozi, Kristo, Bwana

Nyimbo za Dini, 98


0:00 0:00
Introduction
All Verses

1. Yesu, Mkombozi, Kristo, Bwana, Hakika mauti, Umeshinda. Umetoka huko, Kuja kwetu, Na maisha yako Ni dhabihu.

2. Na huu mkate, Tunaula, Twakuwaza wewe, Kwa heshima. Na yale mateso, Pale juu Ni upatanisho Wa kudumu.

3. Tuyanywapo maji, Taratibu, Nyoyo hufurahi, Na kusifu. Tuongoze mpaka Tuelewe, Juu ya uzima Wa milele.