Number 98
Yesu, Mkombozi, Kristo, Bwana
Yesu, Mkombozi, Kristo, Bwana
1. Yesu, Mkombozi,Kristo, Bwana,Hakika mauti,Umeshinda.Umetoka huko,Kuja kwetu,Na maisha yakoNi dhabihu.
2. Na huu mkate,Tunaula,Twakuwaza wewe,Kwa heshima.Na yale mateso,Pale juuNi upatanishoWa kudumu.
3. Tuyanywapo maji,Taratibu,Nyoyo hufurahi,Na kusifu.Tuongoze mpakaTuelewe,Juu ya uzimaWa milele.
Maandishi na muziki: Hugh W. Dougall, 1872–1963