Number 100
Sasa Kwa Ustahifu
Sasa Kwa Ustahifu
1. Sasa kwa ustahifu,Kwa upole sujudu.Tathminia, waziaNiliyokufanyia.Kwa damu yangu nyingi,Na maumivu mengi,Kwa mwili wangu piaNimekushuhudia.
2. Mkate huu kwenu,Ni kama mwili wangu;Maji au divai,Damu msalabani.Nilichofanya, eweMwanadamu usife,Pale Fuvu la Kichwa,Ni kifo kupitia.
3. Shauri moyo wako,Tulia na nduguzo.Wasamehe wengineHata nikusamehe.Kwa sala ya imaniShida zako kabidhi,Na neema ya RohoIwe kisima kwako.
4. Kwenye Kiti cha Enzi,Kwenu ni mtetezi;Upendo wangu kwako,Hata hauna mwisho.Kuwa na utiifu,Daima mwangalifu,Kwangu uwe mwamini,Kwako niwe Mwokozi.
Maandishi: Joseph L. Townsend, 1849–1942
Muziki: Ebenezer Beesley, 1840–1906