1. Mungu kamtuma kwetu— Mpatanishaji Yesu— Kutuelekeza njia Ya kurudi kwake Baba.
2. Na akawa mwanadamu, Akakubali adhabu. Akafa bila hatia, Kuifidia sheria.
3. Upendo mtakatifu! Nastahili kushukuru, Kwamba kwa thabihu yake Nakaa moyoni mwake.
4. Kwa mwenendo anataka Nijiweke kama mwana, Ninyenyekee nifunzwe Na Mtakatifu pekee.
5. Sakramenti twashiriki Dhabihu twatafakari, Kwamba neno twatimiza Na kumkumbuka Bwana.