Number 103
Mungu Kamtuma Kwetu
Mungu Kamtuma Kwetu
1. Mungu kamtuma kwetu—Mpatanishaji Yesu—Kutuelekeza njiaYa kurudi kwake Baba.
2. Na akawa mwanadamu,Akakubali adhabu.Akafa bila hatia,Kuifidia sheria.
3. Upendo mtakatifu!Nastahili kushukuru,Kwamba kwa thabihu yakeNakaa moyoni mwake.
4. Kwa mwenendo anatakaNijiweke kama mwana,Ninyenyekee nifunzweNa Mtakatifu pekee.
5. Sakramenti twashirikiDhabihu twatafakari,Kwamba neno twatimizaNa kumkumbuka Bwana.
Maandishi: Edward P. Kimball, 1882–1937
Muziki: Alexander Schreiner, 1901–1987. © 1948 IRI