Number 114
Njooni kwa Shangwe
Njooni kwa Shangwe
1. Njooni kwa shangwe,Nyote mwaminio!Njooni, mji mwema Bethlehemu.O! Tazameni,Bwana kazaliwa;
Njooni tumwabudu;Njooni tumwabudu;Njooni tumwabudu,Kristo, Bwana.
2. Imbeni kwa shangwe,Enyi malaika;Nyote mkaao juu mbinguni!Sifa kwa Mungu,Utukufu kwake!
Njooni tumwabudu;Njooni tumwabudu;Njooni tumwabudu,Kristo, Bwana.
3. Tunakusalimu,Asubuhi njema;Na utukufu wote uwe kwako.Mwana wa Baba,Sasa kazaliwa;
Njooni tumwabudu;Njooni tumwabudu;Njooni tumwabudu,Kristo, Bwana.
Maandishi: Yamehusishwa na John F. Wade, mnamo mwaka 1711–1786; Yametafsiriwa na Frederick Oakeley, 1802–1880
Muziki: Umehusishwa na John F. Wade