Number 114
Njooni kwa Shangwe
Njooni kwa Shangwe
1. Njooni kwa shangwe,
Nyote mwaminio!
Njooni, mji mwema Bethlehemu.
O! Tazameni,
Bwana kazaliwa;
Njooni tumwabudu;
Njooni tumwabudu;
Njooni tumwabudu,
Kristo, Bwana.
2. Imbeni kwa shangwe,
Enyi malaika;
Nyote mkaao juu mbinguni!
Sifa kwa Mungu,
Utukufu kwake!
Njooni tumwabudu;
Njooni tumwabudu;
Njooni tumwabudu,
Kristo, Bwana.
3. Tunakusalimu,
Asubuhi njema;
Na utukufu wote uwe kwako.
Mwana wa Baba,
Sasa kazaliwa;
Njooni tumwabudu;
Njooni tumwabudu;
Njooni tumwabudu,
Kristo, Bwana.
Maandishi: Yamehusishwa na John F. Wade, mnamo mwaka 1711–1786; Yametafsiriwa na Frederick Oakeley, 1802–1880
Muziki: Umehusishwa na John F. Wade