Number 123
Malaika Kaleta Noeli
Malaika Kaleta Noeli
1. Malaika kaleta noeli
Kwa wachungaji maskini makondeni,
Wakilinda kondoo wao
Usiku wa baridi na giza zito.
Noeli, Noeli, Noeli nzuri!
Amezaliwa Mwokozi!
2. Wakaona mbinguni mwangaza
Wa nyota ya mashariki iking’ara;
Ulileta nuru tukufu,
Ukaendelea siku hadi siku.
Noeli, Noeli, Noeli nzuri!
Amezaliwa Mwokozi!
Maandishi na muziki: Wimbo wa Krismasi wenye utamaduni wa Waingereza, karne ya 17