Book cover

Ifanye Njia Ng’avu

Nyimbo za Dini, 131

0:00 0:00
Introduction
All Verses

1. Ifanye njia ng’avu, Jaza nafsi na nuru, Je, moyo u tayari? Gizani pawe mwanga, Vivuli kutoweka, Kama moyoni unanuru.

Je, moyo u tayari? Toa mwali mng’avu Usiku uwe siku; Utavuna amani, Kama moyoni unanuru.

2. Nena neno tulivu Kwenye moyo wa hofu, Je, moyo u tayari? Wala si jambo dogo, Neema iletwayo, Kama moyoni unanuru.

Je, moyo u tayari? Toa mwali mng’avu Usiku uwe siku; Utavuna amani, Kama moyoni unanuru.

3. Lifanye jambo jema Kwa yule mwenye haja, Je, moyo u tayari? Mzigo mtwalie, Shida mpunguzie Kama moyoni unanuru.

Je, moyo u tayari? Toa mwali mng’avu Usiku uwe siku; Utavuna amani, Kama moyoni unanuru.

4. Kuishi kwa furaha Duniani pa shida, Je, moyo u tayari? Utang’ara upendo, Mtukufu mng’ao, Kama moyoni unanuru.

Je, moyo u tayari? Toa mwali mng’avu Usiku uwe siku; Utavuna amani, Kama moyoni unanuru.