1. Ifanye njia ng’avu,
Jaza nafsi na nuru,
Je, moyo u tayari?
Gizani pawe mwanga,
Vivuli kutoweka,
Kama moyoni unanuru.
Je, moyo u tayari?
Toa mwali mng’avu
Usiku uwe siku;
Utavuna amani,
Kama moyoni unanuru.
2. Nena neno tulivu
Kwenye moyo wa hofu,
Je, moyo u tayari?
Wala si jambo dogo,
Neema iletwayo,
Kama moyoni unanuru.
Je, moyo u tayari?
Toa mwali mng’avu
Usiku uwe siku;
Utavuna amani,
Kama moyoni unanuru.
3. Lifanye jambo jema
Kwa yule mwenye haja,
Je, moyo u tayari?
Mzigo mtwalie,
Shida mpunguzie
Kama moyoni unanuru.
Je, moyo u tayari?
Toa mwali mng’avu
Usiku uwe siku;
Utavuna amani,
Kama moyoni unanuru.
4. Kuishi kwa furaha
Duniani pa shida,
Je, moyo u tayari?
Utang’ara upendo,
Mtukufu mng’ao,
Kama moyoni unanuru.
Je, moyo u tayari?
Toa mwali mng’avu
Usiku uwe siku;
Utavuna amani,
Kama moyoni unanuru.
Maandishi: Helen Silcott Dungan, 1855–1914
Muziki: James M. Dungan, 1851–1925