1. Chagua jema tu kila wakati,
Kwa mema Roho huongoza,
Daima ataangazia nafsi,
Unapochagua jema.
Chagua, jema tu!
Uongozwe na hekima.
Chagua, jema tu!
Mungu akupe baraka.
2. Chagua jema! Na usiruhusu
Uovu hata ukushinde.
Dunia inayo mengi majibu;
Acha Roho aongoze.
Chagua, jema tu!
Uongozwe na hekima.
Chagua, jema tu!
Mungu akupe baraka.
3. Chagua jema, amani upate,
Chagua jema, kuna kinga.
Chagua jema, ufanyapo yote;
Mungu awe lengo jipya.
Chagua, jema tu!
Uongozwe na hekima.
Chagua, jema tu!
Mungu akupe baraka.
Maandishi: Joseph L. Townsend, 1849–1942
Muziki: Henry A. Tuckett, 1852–1918