Number 137
Hesabu Baraka
Hesabu Baraka
1. Wimbi la maisha likutosapo,Unakata tamaa ushindwapo,Hesabu baraka, kwa mojamoja,Wema wa Mungu utakushangaza.
Zihesabu;Kwa mojamoja.Zihesabu;Ona ya Bwana.Zihesabu;Kwa mojamoja.Hesabu baraka;Ona ya Bwana.
2. Je, unaelemewa na mzigo?Msalaba wakushinda uzito?Hesabu baraka; shaka ziishe,Na kisha utaimba siku zote.
Zihesabu;Kwa mojamoja.Zihesabu;Ona ya Bwana.Zihesabu;Kwa mojamoja.Hesabu baraka;Ona ya Bwana.
3. Uwaonapo wengine na mali,Kumbuka ahadi zake Mwokozi.Hesabu baraka; wingi wa pesaHaununui ufalme wa Bwana.
Zihesabu;Kwa mojamoja.Zihesabu;Ona ya Bwana.Zihesabu;Kwa mojamoja.Hesabu baraka;Ona ya Bwana.
4. Hivyo matatizo yakukumbapo,Mungu yupo nawe, usife moyo.Hesabu baraka; na utajaliwaMalaika watakusaidia.
Zihesabu;Kwa mojamoja.Zihesabu;Ona ya Bwana.Zihesabu;Kwa mojamoja.Hesabu baraka;Ona ya Bwana.
Maandishi: Johnson Oatman, Jr., 1856–1922
Muziki: Edwin O. Excell, 1851–1921