Number 139
Tusonge Mbele
Tusonge Mbele
1. Tusonge mbele kwenye kazi ya Bwana,Ndipo tukaipate zawadi tukifa;Katika vita tuushike upanga,Upanga wa ukweli.
Jipe moyo shinda aduiMsihofu, Bwana yu nasiHatutawasikiliza waovuTutamtii Bwana Mungu.
2. Hatutasita ingawa tu wachacheTunapolinganishwa na adui kule;Katika Bwana nguvu yake tupateKutetea ukweli.
Jipe moyo shinda aduiMsihofu, Bwana yu nasiHatutawasikiliza waovuTutamtii Bwana Mungu.
3. Hatutahofu tunapotenda mema,Kwa sababu Bwana yu karibu daima;Katika shida yeye atuwezeshaTuushike ukweli.
Jipe moyo shinda aduiMsihofu, Bwana yu nasiHatutawasikiliza waovuTutamtii Bwana Mungu.
Maandishi na muziki: Evan Stephens, 1854–1930