1. Askari wa Kristo!
Mwendo wa vita!
Msalaba Wake
Watangulia.
Jemadari, Kristo,
Ndiye Mshindi.
Fuata bendera!
Twende vitani.
Askari wa Kristo!
Mwendo wa vita!
Msalaba Wake
Watangulia
2. Panapo ushindi
Shetani mbio;
Askari tusonge,
Ushindi bado.
Adui huhofu
Shangwe za sifa;
Ndugu, tuimbeni,
Sauti paza.
Askari wa Kristo!
Mwendo wa vita!
Msalaba Wake
Watangulia.
3. Kanisa la Mungu
Ni jeshi kuu;
Ndugu, tunapita
Patakatifu.
Hatugawanyiki;
Ni moja umbo;
Katika hisani
Na mafundisho.
Askari wa Kristo!
Mwendo wa vita!
Msalaba Wake
Watangulia.
4. Mbele basi watu,
Jumuikeni.
Sauti ziimbe
Kama washindi:
Sifa na adhama
Kwake Mfalme.
Hivyo malaika,
Watu, waimbe:
Askari wa Kristo!
Mwendo wa vita!
Msalaba Wake
Watangulia.
Maandishi: Sabine Baring-Gould, 1834–1924
Muziki: Arthur S. Sullivan, 1842–1900