1. Askari wa Kristo! Mwendo wa vita! Msalaba Wake Watangulia. Jemadari, Kristo, Ndiye Mshindi. Fuata bendera! Twende vitani.
Askari wa Kristo! Mwendo wa vita! Msalaba Wake Watangulia
2. Panapo ushindi Shetani mbio; Askari tusonge, Ushindi bado. Adui huhofu Shangwe za sifa; Ndugu, tuimbeni, Sauti paza.
Askari wa Kristo! Mwendo wa vita! Msalaba Wake Watangulia.
3. Kanisa la Mungu Ni jeshi kuu; Ndugu, tunapita Patakatifu. Hatugawanyiki; Ni moja umbo; Katika hisani Na mafundisho.
Askari wa Kristo! Mwendo wa vita! Msalaba Wake Watangulia.
4. Mbele basi watu, Jumuikeni. Sauti ziimbe Kama washindi: Sifa na adhama Kwake Mfalme. Hivyo malaika, Watu, waimbe:
Askari wa Kristo! Mwendo wa vita! Msalaba Wake Watangulia.