Book cover

Tazama, Jeshi Kubwa

Nyimbo za Dini, 144

0:00 0:00
Introduction
All Verses

1. Tazama, jeshi kubwaLabeba mkuki,Laenda kupiganaVita vya uhai.Askari majasiriNa nguvu wanazo,Wafuata KamandaNa kuimba wimbo:

Ushindi! Ushindi!Kwake Mkombozi!Ushindi! Ushindi!Kwake Bwana Yesu!Ushindi! Ushindi! Ushindi!Kwake Bwana Yesu!

2. Hata wakikamatwa,Na yule adui,Hawaogopi kamweWana ujasiri.“Muwe waaminifu!”Kamanda asema;Wafuata ishara,Huku wakiimba:

Ushindi! Ushindi!Kwake Mkombozi!Ushindi! Ushindi!Kwake Bwana Yesu!Ushindi! Ushindi! Ushindi!Kwake Bwana Yesu!

3. Vita na migogoro,Vitakapokwisha,Na kukusanywa wotePamoja na Bwana,Mbele yake Mfalme,Lile kusanyikoLitamsifu BwanaNa kuimba wimbo:

Ushindi! Ushindi!Kwake Mkombozi!Ushindi! Ushindi!Kwake Bwana Yesu!Ushindi! Ushindi! Ushindi!Kwake Bwana Yesu!