1. Tazama, jeshi kubwa
Labeba mkuki,
Laenda kupigana
Vita vya uhai.
Askari majasiri
Na nguvu wanazo,
Wafuata Kamanda
Na kuimba wimbo:
Ushindi! Ushindi!
Kwake Mkombozi!
Ushindi! Ushindi!
Kwake Bwana Yesu!
Ushindi! Ushindi! Ushindi!
Kwake Bwana Yesu!
2. Hata wakikamatwa,
Na yule adui,
Hawaogopi kamwe
Wana ujasiri.
“Muwe waaminifu!”
Kamanda asema;
Wafuata ishara,
Huku wakiimba:
Ushindi! Ushindi!
Kwake Mkombozi!
Ushindi! Ushindi!
Kwake Bwana Yesu!
Ushindi! Ushindi! Ushindi!
Kwake Bwana Yesu!
3. Vita na migogoro,
Vitakapokwisha,
Na kukusanywa wote
Pamoja na Bwana,
Mbele yake Mfalme,
Lile kusanyiko
Litamsifu Bwana
Na kuimba wimbo:
Ushindi! Ushindi!
Kwake Mkombozi!
Ushindi! Ushindi!
Kwake Bwana Yesu!
Ushindi! Ushindi! Ushindi!
Kwake Bwana Yesu!
Maandishi: Fanny J. Crosby, 1820–1915
Muziki: Adam Geibel, 1855–1933