1. Mwamba wa wokovu wetu, Mwokozi wa dunia, Kwa imani yetu kuu Twakunjua bendera.
Simameni na bendera; Simameni na nguvu. Ukweli twapigania, Tusake kila siku.
2. Twapambana na maovu; Twapigania haki. Vita kali kila siku; Tufanyie ushindi.
Simameni na bendera; Simameni na nguvu. Ukweli twapigania, Tusake kila siku.
3. Tusonge mbele kwa nyimbo Tukiwa madhubuti; Kila vita tushindayo Tunafanya kwa ari.
Simameni na bendera; Simameni na nguvu. Ukweli twapigania, Tusake kila siku.
4. Baada ya mapigano Kushindia imani, Baada ya migongano Na kumaliza kazi,
Mwamba wa wokovu wetu, Mwokozi wa dunia, Pokea shuhuda zetu Twaikunja bendera.