1. Mwamba wa wokovu wetu,
Mwokozi wa dunia,
Kwa imani yetu kuu
Twakunjua bendera.
Simameni na bendera;
Simameni na nguvu.
Ukweli twapigania,
Tusake kila siku.
2. Twapambana na maovu;
Twapigania haki.
Vita kali kila siku;
Tufanyie ushindi.
Simameni na bendera;
Simameni na nguvu.
Ukweli twapigania,
Tusake kila siku.
3. Tusonge mbele kwa nyimbo
Tukiwa madhubuti;
Kila vita tushindayo
Tunafanya kwa ari.
Simameni na bendera;
Simameni na nguvu.
Ukweli twapigania,
Tusake kila siku.
4. Baada ya mapigano
Kushindia imani,
Baada ya migongano
Na kumaliza kazi,
Mwamba wa wokovu wetu,
Mwokozi wa dunia,
Pokea shuhuda zetu
Twaikunja bendera.
Maandishi: Joseph L. Townsend, 1849–1942
Muziki: William Clayson, 1840–1887