1. Nenda kwa imani, taja Yesu ndiye Kristo, Na ndiye Mwana pekee; Litangaze neno. Nenda kwa matumaini Injili eneza, Kwamba wanadamu wote Ni wana wa Baba.
2. Nenda kawaelezee Udugu ni raha— Kuwa twaweza kuishi Milele pamoja. Nenda uwahudumie, Pasipo malipo; Kisha utafurahia Kazi yake Kristo
3. Nenda kwa nguvu useme Kuna urejesho, Tutaupata uzima Kupitia Kristo. Nenda hubiri ukweli, Amani, furaha, Ili watakaotii Wamsifu Bwana.