Number 150
Nenda kwa Imani
Nenda kwa Imani
1. Nenda kwa imani, tajaYesu ndiye Kristo,Na ndiye Mwana pekee;Litangaze neno.Nenda kwa matumainiInjili eneza,Kwamba wanadamu woteNi wana wa Baba.
2. Nenda kawaelezeeUdugu ni raha—Kuwa twaweza kuishiMilele pamoja.Nenda uwahudumie,Pasipo malipo;Kisha utafurahiaKazi yake Kristo
3. Nenda kwa nguvu usemeKuna urejesho,Tutaupata uzimaKupitia Kristo.Nenda hubiri ukweli,Amani, furaha,Ili watakaotiiWamsifu Bwana.
Maandishi: Ruth M. Gardner, 1927–1999. © 1985 IRI
Muziki: Lyall J. Gardner, 1926–2012. © 1985 IRI