1. Nisomapo maandiko, Baba wa wanadamu. Nijaze moyo hekima, Jaza fikira zangu.
2. Nisomapo maandiko, Niguse roho, Bwana, Nionyeshe maajabu Kila ninaposoma.
3. Nisomapo maandiko, Nionyeshe huruma. Ufariji moyo wangu; Niponye majeraha.
4. Nisomapo maandiko, Nifikiri, nitii. Neno lako ni uzima; Nitembee nuruni.