Number 159
Nisomapo Maandiko
Nisomapo Maandiko
1. Nisomapo maandiko,Baba wa wanadamu.Nijaze moyo hekima,Jaza fikira zangu.
2. Nisomapo maandiko,Niguse roho, Bwana,Nionyeshe maajabuKila ninaposoma.
3. Nisomapo maandiko,Nionyeshe huruma.Ufariji moyo wangu;Niponye majeraha.
4. Nisomapo maandiko,Nifikiri, nitii.Neno lako ni uzima;Nitembee nuruni.
Maandishi na muziki: C. Marianne Johnson Fisher, 1932–2018. © 1985 IRI