1. Wazee wa Israeli twendeni Popote tuwasake wenye haki, Penye jangwa, bahari na misitu, Tuwalete Sayuni wawe huru.
O! Babiloni, Babiloni twakuaga; Milima ya Efraemu twaenda.
2. Mavuno mengi wavunaji haba; Tukiungana yote twayaweza. Tutenganishe nganona magugu Toka kifungoni wawekwe huru.
O! Babiloni, Babiloni twakuaga; Milima ya Efraemu twaenda.
3. Tuwatembelee nao maskini Wenye njaa na wale wenye dhiki; Tuwafariji kwa injili yake Tuwaonyeshe njia ya milele.
O! Babiloni, Babiloni twakuaga; Milima ya Efraemu twaenda.