Number 170
Wazee wa Israeli (Wanaume)
Wazee wa Israeli (Wanaume)
1. Wazee wa Israeli twendeni
Popote tuwasake wenye haki,
Penye jangwa, bahari na misitu,
Tuwalete Sayuni wawe huru.
O! Babiloni, Babiloni twakuaga;
Milima ya Efraemu twaenda.
2. Mavuno mengi wavunaji haba;
Tukiungana yote twayaweza.
Tutenganishe nganona magugu
Toka kifungoni wawekwe huru.
O! Babiloni, Babiloni twakuaga;
Milima ya Efraemu twaenda.
3. Tuwatembelee nao maskini
Wenye njaa na wale wenye dhiki;
Tuwafariji kwa injili yake
Tuwaonyeshe njia ya milele.
O! Babiloni, Babiloni twakuaga;
Milima ya Efraemu twaenda.
Maandishi: Cyrus H. Wheelock, 1813–1894
Muziki: Thomas H. Bayly, 1797–1839, umefanyiwa marekebisho