1. O! Kisima cha baraka, Imbisha moyo wangu; Tiririko za rehema, Zaniita kusifu.
Nifundishe tenzi nzuri, Ziimbwazo uliko; Mlima – wangu msingi — Nasifu pendo lako.
2. Naita Ebenezeri, Hapa nimefikia, Nako kwa yako mapenzi, Nyumbani nitafika.
Kupotea ni mwepesi, Hata kumwacha Mungu; Moyo wangu, Ee Mwokozi, Ufunge kwako juu.
3. Alinitafuta Yesu Nikiwa ugenini; Akamwaga yake damu Kunitoa jangani.
Kupotea ni mwepesi, Hata kumwacha Mungu; Moyo wangu, Ee Mwokozi, Ufunge kwako juu.
4. O! Yanilazimu kuwa Daima mwiwa wako! Ufungavyo wako wema, Nifunge wangu moyo.
Kupotea ni mwepesi, Hata kumwacha Mungu; Moyo wangu, Ee Mwokozi, Ufunge kwako juu.