Number 174
O! Kisima Cha Baraka
O! Kisima Cha Baraka
1. O! Kisima cha baraka,Imbisha moyo wangu;Tiririko za rehema,Zaniita kusifu.
Nifundishe tenzi nzuri,Ziimbwazo uliko;Mlima – wangu msingi —Nasifu pendo lako.
2. Naita Ebenezeri,Hapa nimefikia,Nako kwa yako mapenzi,Nyumbani nitafika.
Kupotea ni mwepesi,Hata kumwacha Mungu;Moyo wangu, Ee Mwokozi,Ufunge kwako juu.
3. Alinitafuta YesuNikiwa ugenini;Akamwaga yake damuKunitoa jangani.
Kupotea ni mwepesi,Hata kumwacha Mungu;Moyo wangu, Ee Mwokozi,Ufunge kwako juu.
4. O! Yanilazimu kuwaDaima mwiwa wako!Ufungavyo wako wema,Nifunge wangu moyo.
Kupotea ni mwepesi,Hata kumwacha Mungu;Moyo wangu, Ee Mwokozi,Ufunge kwako juu.
Maandishi: Robert Robinson, 1735–1790
Muziki: John Wyeth, 1770–1858