Nyimbo Za Dini Pamoja Na Nyimbo Za Watot (1983),
p. 8
Shida Zinapoingia
Shida Zinapoingia
1. Wimbi la maisha likutosapo,
Unakata tamaa ushindwapo,
Hesabu baraka, kwa mojamoja,
Wema wa Mungu utakushangaza.
Zihesabu;
Kwa mojamoja.
Zihesabu;
Ona ya Bwana.
Zihesabu;
Kwa mojamoja.
Hesabu baraka;
Ona ya Bwana.
2. Je, unaelemewa na mzigo?
Msalaba wakushinda uzito?
Hesabu baraka; shaka ziishe,
Na kisha utaimba siku zote.
Zihesabu;
Kwa mojamoja.
Zihesabu;
Ona ya Bwana.
Zihesabu;
Kwa mojamoja.
Hesabu baraka;
Ona ya Bwana.
3. Uwaonapo wengine na mali,
Kumbuka ahadi zake Mwokozi.
Hesabu baraka; wingi wa pesa
Haununui ufalme wa Bwana.
Zihesabu;
Kwa mojamoja.
Zihesabu;
Ona ya Bwana.
Zihesabu;
Kwa mojamoja.
Hesabu baraka;
Ona ya Bwana.
4. Hivyo matatizo yakukumbapo,
Mungu yupo nawe, usife moyo.
Hesabu baraka; na utajaliwa
Malaika watakusaidia.
Zihesabu;
Kwa mojamoja.
Zihesabu;
Ona ya Bwana.
Zihesabu;
Kwa mojamoja.
Hesabu baraka;
Ona ya Bwana.
Maandishi: Johnson Oatman, Jr., 1856–1922
Muziki: Edwin O. Excell, 1851–1921
Maandishi: Johnson Oatman, Jr., 1856–1922
Muziki: Edwin O. Excell, 1851–1921