Page 15
Kuna Mlima Wa Kijani
Kuna Mlima Wa Kijani
1. Nje ya Yerusalemu
Kilimani kule,
Alisulubiwa Kristo
Kuokoa sote.
2. Hatuwezi kuelewa
Yake maumivu,
Aliteswa, twaamini,
Kwa ajili yetu.
3. Hapakuwa na mwingine,
Wa kulipa deni.
Yeye kafungua lango
Tufike mbinguni.
4. Alitupenda kwa dhati!
Nasi tumpende!
Damu yake tusadiki,
Na tumfuate.
Maandishi: Cecil Frances Alexander, 1818–1895
Muziki: John H. Gower, 1855–1922