Page 1
Niambie Ukweli Ni Nini
Niambie Ukweli Ni Nini
1. Ukweli ni nini? ThamaniyeHuzidi vito na dhahabu,Na ubora utaonekana paleAmbapo utajiri wote wa falmeUtaonwa kama uchafu.
2. Ukweli ni nini? Tuzo zuriWatu na mbingu kuwania.Utafute ung’aripo kilindini,Au ufukuzie hadi mbinguni:Ni lengo la kutamaniwa.
3. Mwonevu nguvu atazidiwaAtaposhindana na haki.Hivyo ukweli utadumu daima,Na ngome yake kuhimili vimbungaNa mapinduzi ya katili.
4. Hivyo, ukweli ni mwisho na mwanzo,Msimu, nyakati hauna.Japo mbingu, nchi zitafika mwisho,Ukweli, uhalisi, utakuwepo,Kubakia hivyo, daima.
Maandishi: John Jaques, 1827–1900
Muziki: Ellen Knowles Melling, 1820–1905