Nyimbo Za Dini Pamoja Na Nyimbo Za Watot (1983),
p. 30
Tufurahi Ni Sasa
Tufurahi Ni Sasa
1. Tuishangilie siku ya wokovu,Sisi sio wageni duniani.Habari njema, mataifa na watu,Wokovu waja hivi karibuni.Ahadi kwa Wema zitapotimizwa,Nao hawatasumbuliwa tena,Kama Edeni, dunia itakuwa,Yesu atasema, “Njoo nyumbani.”
2. Sote tutapendana bila ghadhabu,Tutaungana na kuacha dhambi.Na wakati wakiogopa waovu,Tutangojea siku ya Mwokozi.Ahadi kwa Wema zitapotimizwa,Nao hawatasumbuliwa tena,Kama Edeni, dunia itakuwaYesu atasema, “Njoo nyumbani.”
3. Tutaamini mkono wa YehovaKutuongoza nyakati za mwisho.Uangamizaji utakapoisha,Tutafufuka Mfalme ajapo.Ahadi kwa Wema zitapotimizwa,Watatunukiwa na malaika,Kama Edeni, dunia itakuwa,Na Wema wataungana na Kristo.
Maandishi: William W. Phelps, 1792–1872. Yalijumuishwa katika kitabu cha kwanza cha nyimbo za Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 1835.
Muziki: Henry Tucker, 1826–1882
Maandishi: William W. Phelps, 1792–1872. Yalijumuishwa katika kitabu cha kwanza cha nyimbo za Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 1835.