1. Labda siyo kwenye milima
Wala penye tufani,
Labda siyo mbele ya vita
Bwana anihitaji.
Akiniita, kwa upole
Nipite njia mpya,
Nitajibu, Bwana, Mwaminifu:
Utakako, nitakwenda.
Nitakwenda utakako, Bwana,
Milimani hata ng’ambo;
Nitasema utakacho, Bwana;
Nitakuwa utakavyo.
2. Labda leo kuna maneno
Natakiwa niseme;
Labda kwenye njia za dhambi
Yupo asumbukaye.
Mwokozi wangu, niongoze,
Njiani penye giza,
Ili nitangaze neno tamu;
Utakacho, nitasema.
Nitakwenda utakako, Bwana,
Milimani hata ng’ambo;
Nitasema utakacho, Bwana;
Nitakuwa utakavyo.
3. Kuna mahali duni hasa
Huko kwa walimwengu
Pa kwenda kufanyia kazi
Kwa ajili ya Yesu.
Hivyo najikabidhi kwako,
Nikijua napendwa,
Hili nafanya kwa moyo wote:
Utakavyo, nitakuwa.
Nitakwenda utakako, Bwana,
Milimani hata ng’ambo;
Nitasema utakacho, Bwana;
Nitakuwa utakavyo.
Maandishi: Mary Brown, 1856–1918
Muziki: Carrie E. Rounsefell, 1861–1930