Page 46
Ulipoondoka Nyumbani Leo Asubuhi
Ulipoondoka Nyumbani Leo Asubuhi
1. Ulipoamka leo,
Je, uliomba?
Katika jina la Kristo,
Kusihi upendeleo
Ili kulindwa?
Jinsi sala hufariji!
Nuru huongezeka.
Punde ukiwa gizani,
Kumbuka sala.
2. Ulipopata hasira,
Je, uliomba?
Upewe neema, ndugu,
Wengine usihukumu,
Waliokosa?
Jinsi sala hufariji!
Nuru huongezeka.
Punde ukiwa gizani,
Kumbuka sala.
3. Ulipopatwa na shida,
Je, uliomba?
Ulipojawa huzuni,
Malhamu ya Gileadi
Ulitafuta?
Jinsi sala hufariji!
Nuru huongezeka.
Punde ukiwa gizani,
Kumbuka sala.
Maandishi: Mary A. Pepper Kidder, 1820–1905
Muziki: William O. Perkins, 1831–1902